PeerCorps Trust Fund (PEERCORPS) Asasi ya kijamii,
isiyo jikita kwenye siasa, isiyo ya kiserikali, na
iliyosajiliwa na serikali ya muungano wa Tanzania, chini ya
sheria ya wadhamini Tanzania, kipengele 375 cha sheria za
Tanzania. Ilifanikiwa kuwa ushirika nchini Tanzania mnamo
tarehe 19 Aprili 2004 na kupewa cheti cha incorporation
namba (2823). PeerCorps inapigania kuweka tofaouti katika
maisha ya vijana walioko kwenye hatari ya kudhuriwa, watoto
na wanawake vijinini na kitaifa.
PeerCorps inapigaia fadhila ya sera na utaratibu/mpango
kwa ajili ya vijana, wanawake na watoto haswa wanaishi
maeneo ya ngazi ya chini, ili kuboresha maisha yao.
Tunafuatilia mambo yanayohusika na virusi vya UKIMWI,
malaria, kifua kikuu, uzazi na afya ya watoto na kutumia
madawa ya kulevya kutoka katika jamii. Tunasaidia au
kurahisisha na kuhimili mradi inayosaidia ubora wa maisha
wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, na kuendeleza
miradi inayosisitiza na kupa kipaumbele kwa vijana wenye
mahitaji ya kipekee kama vile watoto wa mtaa, yatima,
makahaba, wakimbizi na wanajeshi.